[Tprisf] Naomba msaada - utaratibu mpya wa ukodishwaji wa magari ya Taasisi kwa kazi za kitafiti

Mwema Felix mwema.felix at gmail.com
Tue Mar 5 09:47:26 EAT 2013


Habari za kazi,

Natumai mtakua mnataarifa au kuona tangazo linalohusu utaratibu mpya wa
ukodishwaji wa magari ya Taasisi kwa shughuri za kitafiti. Utaratibu huu
umeanza kutumika mwezi huu wa tatu 2013.

Naomba msaada wenu; kuna baadhi ya wanasayansi ambao wameandika miradi na
kutuma kwa wahisani (proposals) ili kupatiwa fedha (mfano - miezi sita
iliyopita mpaka sasa). Bajeti ya usafiri iliyokadiriwa kwenye miradi yao ni
kulingana na utaratibu uliokuwa unatumika hapo awali (*sio huu wa kulipia
USD 0.4/km*).

Sasa endapo wanasayansi hao wakafanikiwa kupata pesa hizo na kwa utaratibu
huu mpya wa ukodishwaji magari:-

   1. hali itakuwaje?
   2. mwanasayansi husika atatoa wapi hela za kukodishia gari husika kwa
   utaratibu huu mpya wakati gharama hii mpya haikuwepo kwenye bajeti yake?
   3. viongozi wa taasisi wameliona suala hili?
   4. wanasayansi watakaopatwa na shida hii (yawezekana ukawa ni wewe)
   watasaidiwaje?
   5. sisi kama wanasayansi - tunafanyaje sasa?

Kuna miradi ambayo teyari ipo inaendelea na nina uhakika utaratibu huu mpya
utaathiri kazi zao za kitafiti kwa namna moja au nyingine. Na wao
watafanyaje? Watatoa wapi pesa za kulipia magari hayo wakati gharama hizi
mpya hazikuwa kwenye bajeti zao?

Mimi nashauri (mtazamo wangu tu), utaratibu huu mpya wa ukodishwaji wa
magari kwa kulipia dola 0.4 kwa kilomita uanze kutumika kwa miradi mipya!
Mfano, wanasayansi watakao andika miradi kuanzia sasa basi watumie viwango
hivi vipya kwenye bajeti za miradi yao.

Nategemea kusoma mchango wako.

Wako katika kazi

Mwema
-------------- next part --------------
An HTML attachment was scrubbed...
URL: <http://lists.habari.co.tz/pipermail/tprisf/attachments/20130305/aa3f44d6/attachment-0001.html>


More information about the Tprisf mailing list