[Tprisf] Fwd: [wanabidii] Viwango vipya vya nauli kwa usafiri wa mijini na mikoani
Mwema Felix
mwema.felix at gmail.com
Wed Apr 3 11:55:12 EAT 2013
Dear all,
This may be important for you to know.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha
mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini
na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya
kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi
na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya
kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia
tarehe 12 Aprili, 2013.
SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa
maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na
huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji.
Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya
kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika
kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi
rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo
makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy
Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio
ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini
(Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la
gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.
Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya
nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu
waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.
Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA
iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu
maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi
ya mwisho.
Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16 Cha
Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa
mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma,
faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za
huduma inayotolewa.
Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti,
haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa
vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za
usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli
za Daladala kwa wastani wa 24.46%.
Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa
mabasi ya kawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi
ya daraja la juu.
Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:
1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam
**
**
Umbali wa Njia
Kiwango Kipya cha Nauli
Mfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
Sh 400/=
Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15
Sh 450/=
Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20
Sh 500/=
Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25
Sh 600/=
Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30
Sh 750/=
Kibamba – Kariakoo
Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo
yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz
Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima
ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia
zote za Jiji la Dar es Salaam.
2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu
**
**
Daraja la Basi
Nauli ya zamani kwa km-abiria
Nauli mpya kwa km-abiria
Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia
Basi la Kawaida kwa njia ya lami
Sh 30.67
Sh 36.89
DSM–Mbeya Km 833
Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi
Sh 37.72
Sh 46.11
S/wanga-KigomaKm 551
Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi Luxury
Sh 45.53
Sh 53.22
DSM–Mwanza Km 1,154
Sh 61,400
Basi la hadhi ya juu (Luxury)
Sh 51.64
Sh 58.47
DSM–Arusha Km 616
Sh 36,000
Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora
wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya
masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama
ifuatavyo:
1. Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za
safari
2. Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za
Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza
kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango
vya nauli
3. Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
4. Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja
husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora
Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:
1. Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
2. Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha
safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina
yoteyote kwa abiria
3. Kutokutumia wapiga debe
4. Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa
karibu na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka
za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla,
katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa
kiwango cha juu.
*A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013*
[image: Picture]
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2PKzie19C
-------------- next part --------------
An HTML attachment was scrubbed...
URL: <http://lists.habari.co.tz/pipermail/tprisf/attachments/20130403/1f9d746b/attachment-0001.html>
More information about the Tprisf
mailing list